Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, June 8, 2013

Sisitizo la Ethiopia la kujenga bwawa la an Nahdha

Serikali ya Ethiopia imepuuza malalamiko yanayotolewa na serikali ya Misri na imesisitiza juu ya kuendelea na ujenzi wa bwawa la an Nahdha. Msemaji wa Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa, malalamiko yanayotolewa na Misri ya kuitaka Ethiopia isitishe ujenzi wa bwawa hilo hayakubaliki. Hayo yanaelezwa katika hali ambayo, Essam Haddad mshauri wa masuala ya kigeni wa Rais Muhammad Morsi wa Misri  amesema kuwa, Cairo haitatumia njia  za kijeshi kwa lengo la kuukwamua mgogoro wa bwawa la an Nahdha. Imeelezwa kuwa, ujenzi wa bwawa hilo utasababisha kupungua hisa ya Misri ya karibu cubic miter bilioni 55 na milioni 500 ya maji kila mwaka, kwa mujibu wa makubaliano ya kimataifa yaliyotiwa saini mwaka 1929 na 1959.  Wataalamu wa masuala ya kilimo wanasema kuwa, hatua ya ghafla ya Ethiopia ya kuweka mkondo mpya wa maji ya Mto Nile na yatakayoelekea kwenye bwawa hilo, utasababisha athari  kubwa katika sekta ya kilimo katika nchi za Misri na Sudan.

No comments: