Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani shambulizi
la waasi wa al Shabab lililolenga ofisi ya umoja huo nchini Somalia.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Martin Nesirky ameeleza kuwa, Ban
Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa haupaswi kuvunjwa moyo katika
kutekeleza majukumu yake nchini Somalia na kwamba utaendelea na mipango
yake ya kuwasaidia Wasomali.
Katika shambulizi hilo, al Shabab walitega
bomu kwenye gari nje ya ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu
Mogadishu ambapo watu 15 waliouawa. Miongoni mwa waliouawa ni afisa wa
UNDP, makandarasi watatu kutoka Afrika Kusini na walinzi wanne wa
Kisomali.
Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulihamishia shughuli zake mjini
Mogadishu kutoka nchi jirani ya Kenya, baada ya kuwa huko kwa miaka
mingi kutokana na hofu ya usalama. Hii ni mara ya kwanza ofisi za Umoja
wa Mataifa kushambuliwa mjini Mogadishu, tangu taasisi hiyo ilipoanza
shughuli zake nchini Somalia.







No comments:
Post a Comment