Watu wasiopungua 50 wameuawa na wanamgambo wenye silaha katika
eneo la Zamfara nchini Nigeria. Imeripotiwa kuwa watu karibu 50 wenye
silaha walizingira eneo hilo jana mapema asubuhi na kumlenga kwa risasi
kila mtu mzima aliyeonekana kwenye eneo hilo. Miongoni mwa waliouawa ni
imamu na kiongozi wa eneo hilo.
Wakati huo huo watu 32 wameuawa katika eneo la Maiduguri jimbo la
Borno. Mauaji hayo yamefanywa na watu wanodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la
Boko Haram katika mashambulizi tofauti. Polisi imeripoti kuwa
mashambulizi hayo ya kigaidi yalifanywa dhidi ya shule ya msingi na ya
sekondari kwenye eneo hilo na kushambuliwa wanafunzi waliokuwa wakifanya
mitihani. Tangu Mei 15 jeshi la Nigeria linajitahidi kukabiliana na
wafuasi wa Boko Haram nchini humo.







No comments:
Post a Comment