Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 20, 2013

Ethiopia: Kikao cha Mto Nile kimefanikiwa

Waziri Mshauri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia amesema kuwa, kikao kati ya Tedros Adhanom Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo na mwenzake wa Misri Kamel Amr kuhusiana na ujenzi uliozusha mjadala wa bwawa katika Mto Nile kimefanyika vizuri na kwa mafanikio. Ameongeza kuwa, wanaamini kuwa iwapo maji ya Mto Nile yatatumiwa kwa maslahi ya pande zote, yanaweza kukidhi mahitaji ya nchi zote zilizoko pambizoni mwa mto huo na kubaki.

Hatua ya Ethiopia ya kuamua kujenga bwawa kubwa katika Blue Nile ili kuzalisha umeme imezusha mvutano na Misri ambayo inahofia kuwa ujenzi huo utapunguza fungu lake la maji ya Mto Nile.

No comments: