Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema
kuwa ujumbe wa Mtume Mtukufu SAW ulikuwa ni kuwaokoa walimwengu wote.
Akizungumza mbele ya viongozi wa mfumo wa Kiislamu, mabalozi wa nchi za
Kiislamu walioko Tehran kwenye Husseiniya ya Imam Khomeini MA, Rais
Ahmadinejad amesema kuwa, ujumbe mkuu wa Mtume SAW ulikuwa ni kumuongoza
mwanadamu na shakhsia huyo aliweza kukabiliana na vikwazo mbalimbali
katika kufanikisha ujumbe huo. Katika sehemu nyingine ya hotuba yake,
Rais Ahmadnejad amesema kuwa, mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
yaliyoongozwa na Imam Khomeini MA, yalikuwa yakiwalingania watu kufuata
njia ya saada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa, uadilifu
kamili upatatikana baada ya kudhihiri Imam wa Zama 'Mwenyezi Mungu
aharakishe kudhihiri kwake.'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment