Katika eneo la makaburi ya Kanisa la Mtakatifu Monica yaliyopo katika
Kata ya Kihonda nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro juzi Alhamisi
yaligeuka ukumbi wa disko baada ya baadhi ya vijana kuanza kuimba nyimbo
mbalimbali za aliyekuwa msanii wa kizazi kipya marehemu Albert Mangwea
huku wakicheza.
Katika eneo hilo pia kulitokea uharibifu wa
kuvunjika kwa misalaba iliyotokana na baadhi ya waombolezaji kusimama
juu ya misalaba hiyo na kusababisha uharibifu huo.
Wakati huohuo mratibu wa chama cha msalaba
mwekundu mkoa wa Morogoro Wille Mathew alithibitisha watu 15 kupoteza
fahamu kutokana msongamano wa wananchi waliohudhuria wakati wa kuaga
mwili wa msanii huyo. Mazishi ya Ngwea aliyefariki Afrika Kusini wiki
iliyopita yalihitimishwa majira ya saa kumi alasiri.







No comments:
Post a Comment