Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa,
serikali yake itaendelea na mpango wa ujenzi katika bustani mashuhuri ya
Gezi mjini Istanbul licha ya kuendelea maandamano makubwa ya kupinga
mipango hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari nchini Tunisia, Erdogan
amesema wageni ndio wanaochochea maandamano hayo na kwamba raia kadhaa
wa kigeni wamekamatwa. Hii ni katika hali ambayo, afisa mmoja wa polisi
amefariki dunia leo Alhamisi baada ya kushambuliwa na waandamanaji wenye
hasira mjini Istanbul. Matamshi ya Erdogan yamesababisha mtikisiko
mkubwa wa kiuchumi kwani Lira ya Uturuki imepoteza dhamani dhidi ya dola
huku hisa za serikali zikipungua thamani punde baada ya kutolewa kauli
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment