Kwa mara nyingine serikali ya Congo Brazzaville, imesisitizia udharura
wa kufanyika uchaguzi wa serikali za mitaa. Hayo yalisemwa jana usiku na
mwakilishi wa serikali ya Congo Brazzaville ambaye alitabiri kufanyika
uchaguzi huo mwezi Julai mwaka huu. Séraphin Ondélé ambaye pia ni moja
ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo aliyasema hayo
katika ufunguzi wa kikao cha wanaharakati wa jumuiya za kiraia
kilichofanyika kwa lengo la kuandaa mazingira ya kufanyika uchaguzi huo
na kutekeleza maoni ya wapiga kura nchini humo. Kikao hicho
kilifadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa PNUD. Itakubukwa
kuwa, uchaguzi huo uliakhirishwa, katika mazungumzo ya kisiasa
yaliyofanyika tarehe 23 hadi26 mwezi Machi mwaka huu, mjini Dolisie,
moja ya miji muhimu ya Congo Brazzaville.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment