Harakati ya Kitaifa ya Ukombozi ya Azawad ambayo ni moja ya makundi ya
upinzani nchini Mali, imetangaza kuwa, haitonyamazia kimya shambulizi
lolote la majeshi ya nchi hiyo kama ambavyo pia haitokubali kuweka chini
silaha. Harakati hiyo imesisitiza kuwa, wapiganaji wake hawatoweka
chini silaha zao na wala kunyamazia kimya mashambulizi ya askari wa
serikali dhidi ya maeneo ya mji wa Anefis, wa kusini mwa jimbo la Kidal,
kaskazini mwa Mali. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mossa Ag
Attaher, Msemaji wa harakati hiyo amesisitiza kuwa, Harakati ya Kitaifa
ya Ukombozi ya Azawad, haitaweka chini silaha zake maadamu hali ya
usalama haijarejea katika maeneno ya kaskazini mwa Mali. Ni vyema
kukumbusha kuwa, viongozi wa serikali ya Bamako na wawakilishi wa
harakati hiyo wanatazamiwa kukaa kwenye meza moja ya mazungumzo mjini
Ouagadougou, Burkina Faso kwa lengo la kujadili mgogoro wa nchi hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment