Idadi ya wahanga wa shambulizi lililotekelezwa na kundi la
Ash-Shabab mjini Mogadishu Somalia, dhidi ya ofisi ya Umoja wa Mataifa,
imeongezeka na kufikia watu 18.
Duru za habari kutoka hospitali ya Somalia zimearifu kuwa, idadi ya
wahanga wa shambulio hilo imeongezeka na kufikia watu 18 baada ya
kufariki dunia raia wengine watatu mapema leo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo
wahanga wanne wa shambulizi hilo lililotokea jana ni raia wa kigeni
huku wengine saba wakiwa raia wa Somalia.
Baada ya shambulizi hilo askari wa Umoja wa Afrika kwa kushirikiana
na wale wa Somalia, walifanikiwa kudhibiti jengo hilo la Umoja wa
Mataifa ambalo lilikuwa limedhibitiwa na wanamgambo wa Ash-Shabab na
kuwaua saba kati yao.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amelaani shambulizi la
waasi wa al Shabab lililolenga ofisi ya umoja huo nchini Somalia. Hivi
karibuni Umoja wa Mataifa ulihamishia shughuli zake mjini Mogadishu
kutoka nchi jirani ya Kenya, baada ya kuwa huko kwa miaka mingi kutokana
na hofu ya usalama.







No comments:
Post a Comment