Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya an-Nahdha ya Tunisia
amekosoa vikali fatwa za Yusuf Qardhawi, Mkuu wa Umoja wa Maulama wa
Kiislamu za kuhalalisha vita dhidi ya jeshi la Syria.
Abdelfattah Mourou amekosoa vikali fatwa hizo na kusema kuwa, Sheikh
Qardhawi amekosea vikali kutoa fatwa ya kuhalalisha vita dhidi ya
utawala wa Rais Bashar al-Assad wa Syria na kwamba, hazina mashiko
yoyote katika misingi ya dini ya Kiislamu.
Aidha Naibu Katibu Mkuu wa
Harakati ya an-Nahdha ya Tunisia, amesisitizia udharura wa kukomeshwa
fatwa kama hizo huku akimtaka Qardhawi kurejea kwenye misingi asili ya
dini tukufu ya Kiislamu. Sheikh Abdelfattah Mourou amewataka mashekhe
wengine wanaotoa fatwa mbaya kama hizo wabadilishe mienendo yao ili
kusitisha umwagaji damu wa Waislamu wenzao huko nchini Syria.
Hivi karibuni Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri, kilitoa tamko la
maulama wa kidini akiwemo Yusuf Qardhawi mwenyewe, kikipinga wito wa
kile kinachosemwa eti ni jihadi nchini Syria na kwamba, chuo hicho
hakijawahi kuunga mkono wala kutia saini wito huo.







No comments:
Post a Comment