Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 20, 2013

Hamdallah amkabidhi Abbas barua ya kujiuzulu

Waziri Mkuu mpya wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Rami Hamdallah amemkabidhi Rais wa mamlaka hiyo, Mahmoud Abbas barua ya kujiuzulu kutokana na kile kinachotajwa kuwa mkwaruzano kati yake na manaibu wake wawili.
Hatua hiyo ya Hamdallah imewashangaza wengi kwani hajamaliza hata majuma mawili tangu alipoapishwa. Duru za karibu na msomi huyo zinaarifu kuwa, manaibu wake wawili wamekuwa wakihujumu juhudi zake za kuunda serikali ya umoja wa kitaifa huko Palestina.

Rami Hamdallah aliteuliwa kuchukua nafasi ya mtangulizi wake, Salam Fayadh aliyejiuzulu mwezi Aprili. Haijabainika iwapo Mahmoud Abbas amekubali barua hiyo ya kujiuzulu au la.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Rami Hamdallah alikuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha al-Najah kilichoko katika eneo la Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan katika ardhi za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

No comments: