Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, June 20, 2013

Sudan Kusini yasaini mkataba wa Mto Nile

Habari kutoka Juba nchini Sudan Kusini zinasema kuwa serikali ya nchi hiyo imesaini mkataba wa ugawanaji sawa maji ya Mto Nile.
Mkataba huo unachukua nafasi ya ule wa nyakati za ukoloni ambapo Misri na Sudan ndizo zilizopewa haki ya kunufaika na sehemu kubwa ya maji ya mto huo. Sudan Kusini imekuwa nchi ya 7 kusaini mkataba huo. Nchi zingine ambazo tayari zimesaini makubaliano hayo ni Ethiopia, Rwanda, Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi.

Mkataba huo umekuwa chanzo cha mgogoro wa hivi karibuni kati ya Misri na Ethiopia. Addis Ababa inatumia vipengee vya mkataba huo kujenga bwawa kubwa linalotarajiwa kupunguza kiwango cha maji kinachofika Misri. Jambo hilo limeikasirisha mno serikali ya Cairo ambayo imeapa kutumia uwezo wake wote kuzuia ujenzi wa bwawa hilo.
Hatua ya Sudan Kusini ya kusaini mkataba huo inatarajiwa kuzidisha hitilafu zilizoko kati yake na nchi jirani ya Sudan.

No comments: