Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amesema
kuwa, kuiunga mkono Syria ni kuunga mkono mapambano dhidi ya utawala
bandia wa Israel.
Sheikh Naim Qasim amesema Hizbullah haina lengo jingine ghairi ya
kudumisha muqawama katika eneo la Mashariki ya Kati na kukabiliana na
chokochoko za Israel sambamba na kukata mikono ya magaidi. Akiashiria
kwamba, harakati hiyo haina nia nyingine katika vita vya Syria zaidi ya
muqawama amefafanua kuwa, wapiganaji wa Hizbullah wamesimama imara
kukabiliana na waitifaki wa Marekani, Israel na makundi ya kigaidi
katika eneo hili.
Sheikh Naim Qasim amesisitizia udharura wa kutatuliwa mgogoro wa
Syria kwa njia za kisiasa na maelewano kati ya makundi yote hasimu ili
kwa njia hiyo waweze kuvunja njama za maadui wa taifa hilo la Kiarabu.
Amesema matukio ya Syria yanajiri chini ya njama dhidi ya Lebanon na
eneo kwa ajili ya kuanzishwa Mashariki ya Kati mpya kwa manufaa ya
Israel.







No comments:
Post a Comment