![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amesema kuwa, wananchi wanapaswa
kutumia fursa za kiuchumi zilizoko ili kulisukuma mbele gurudumu la
maendeleo ya nchi yao. Akizungumza wakati wa kuzindua barabara mpya ya
Tanga-Horohoro yenye urefu wa kilometa 65, Rais Kikwete amesema kuweko
miundombinu bora ni wenzo muhimu katika ukuaji wa uchumi. Amewataka
Watanzania kutumia barabara zilizotengenezwa kuboresha maisha yao ya
kila siku na vilevile kuboresha uchumi wa nchi. Kiongozi huyo ameahidi
kwamba serikali yake itaendeleza sera ya kuboresha miundombinu ili
ifikapo mwaka 2015, awe ametekeleza ahadi yake aliyoitoa ya kujenga
barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilomita 11,000. Baadhi ya
mashirika ya kijamii yamejibu mwito wa rais kwa kumtaka ashughulikie
suala la ulaji rushwa kwanza ndani ya serikali yake iwapo kweli ana nia
ya kuboresha uchumi wa Tanzania.







No comments:
Post a Comment