Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 14, 2013

Baraza la mpito CAR lamchagua Djotodia kuwa rais

Baraza la Mpito katika Jamhuri ya Afrika ya Kati limemuidhinisha kiongozi wa kundi la SELEKA, Michael Djotodia kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo. Baraza hilo lenye wanachama 105 limemuidhinisha baada ya kukosekana mpinzani. Mwezi uliopita, Djotodia aliwaongoza waasi wa SELEKA kuipindua serikali ya Rais Francois Bozize ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Benin.
Umoja wa Afrika pamoja na taasisi zingine za kimataifa zilikataa kumtambua kiongozi huyo wa waasi na badala yake akatakiwa kuunda baraza la mpito litakalokuwa na jukumu la kuandaa uchaguzi mkuu baada ya mwaka mmoja. Haijabainika iwapo jamii ya kimataifa itamtambua Djotodia baada ya kuidhinishwa rasmi na baraza hilo la mpito au la. Punde baada ya kuidhinishwa, kiongozi huyo wa SELEKA ameahidi kwamba hatogombea urais wakati wa uchaguzi mkuu.

No comments: