Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanyia majaribio makombora matatu mapya.
Naibu Kamanda wa kikosi hicho Kiumars Heidari amesema makombora hayo
yaliyotengenezwa katika viwanda vya kijeshi hapa Iran yalifanyiwa
majaribio yaliyofanya katika mazoezi ya hivi karibuni ya kikosi cha nchi
kavu. Kamanda huyo amebainisha kuwa makombora hayo ni ya ardhi kwa
ardhi.
Heidari ameongeza kuwa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran kitazindua magari mapya ya deraya Aprili 18 kwa mnasaba
wa Siku ya Jeshi la Iran. Kamanda huyo ameashiria vitisho vya maaduui
dhidi ya Iran na kuonya kuwa Iran itatoa pigo kubwa kwa adui yeyote
atakayethubutu kuanzisha uchokozi. Wakati huo huo kamanda wa Jeshi la
Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari
amesema mwezi ujao Iran itazindua meli mpya ya kivita.
Mwezi uliopita Iran ilizindua meli mpya ya kivita ijulikanayo kama
Jamaran 2 itakayohudumu katika Bahari ya Kaspi. Manowari hizo za kisasa
kabisa za zimetengenezwa kikamilifu hapa Iran kwa kutegemea wahandisi na
wataalamu Wairani pasina msaada wa kigeni.







No comments:
Post a Comment