Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 14, 2013

Wanaokimbia vita Mali waongezeka

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema hali bado ni tete nchiniMali huku watu wakiendelea kukimbia na maelfu wakihitaji msaada ya dharura. Katika taarifa mashirika hayo,ambayo ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu , Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudimia Wakimbizi UNHCR,  yamesema yanajitahidi kwa kila njia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wa Mali. Mashirika hayo yanatumai kuwafikia mamilioni ya watu kwa msaada wa chakula wakiwemo wakimbizi wa ndani 270,000.
WFP imesema linawafikia watu 310,00 kila mwezi kaskazini mwa nchi hiyo. Hata hivyo mashirika hayo yanasema fedha za msaada hazitoshi kukidhi mahitaji yote ya waathirika wa machafuko Mali. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu linasema limeanzisha miradi kadhaa  na kutenga dola milioni 16 kutoka mfuko wa dharura . Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema vita vya Mali vimepelekea kuibuka maafa ya kibinaadamu ambapo maelfu ya watu wameachwa bila makao. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International linasema kumeshuhudiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na mauaji ya watoto katika vita vya Ufaransa nchini Mali. Ufaransa ilianzisha vita nchini Mali Januari 11 mwaka huu kwa kisingizio cha kukabiliana na waasi eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Weledi wa mambo wanasema lengo kuu la hujuma ya Ufaransa huko Mali ni kupora utajiri wa nchi hiyo hasa mafuta ya petroli, dhahabu na madini ya urani.

No comments: