Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 14, 2013

Askari wa Marekani wapambana na wafungwa Gtmo

Askari wamepambana na wafungwa waliosusia chakula katika jela ya kuogofya ya Jeshi la Marekani ya Guantanamo Bay, Cuba.
Taarifa rasmi zinasema ghasia ziliibuka pale wanajeshi wa Marekani walipojaribu kuwapelekea wafungwa katika seli binafsi kila moja. Mawakili wanaowatetea wafungwa katika jela ya Guantanamo huko Cuba inayosimamiwa na Marekani wamesema kuwa baadhi ya wafungwa waliogoma kula chakula wataaga dunia iwapo wataendelea kususia chakula.
Mawakili hao wamesema kuwa wanasikitishwa na hali mbaya za wafungwa hao walioanza mgomo wa kutokula chakula Februari 6 mwaka huu. Wamesema pia kwamba wafungwa wengi waliogoma kula wamepungua sana uzito wa mwili na kwamba sasa wanalishwa kwa nguvu kupitia puani. Watetetezi wa haki za binadamu jana walifanya maandamano makubwa katika miji zaidi ya 26 na majimbo 19 ya Marekani katika kuadhimisha "Siku ya Kuchukua Hatua ya Kuifunga Jela ya Guantanamo na Kuhitimisha Kuwashikilia Washukukiwa Kusiko na Mwisho."

No comments: