Katika hali ambayo Misri inaendelea kukabiliwa na maandamano na
machafuko, bunge la nchi hiyo limeidhinisha nakala iliyofanyiwa
marekebisho ya sheria ya uchaguzi. Rasimu hiyo ya sheria za uchaguzi
inapasa kwanza kuwasilishwa kwenye Mahakama Kuu ya Katiba ya Misri ili
kupasishwa. Mahakama Kuu ya Katiba pia inapasa kuichunguza rasimu hiyo
katika muda wa siku 45 na baadaye kuipasisha au kupinga.
Bunge la Misri limeafiki sheria mpya ya uchaguzi katika hali ambayo Harakati ya Ukombozi wa Kitaifa ya nchi hiyo ingali inaipinga sheria hiyo na imetishia kususia uchaguzi wa bunge. Uchaguzi wa bunge wa Misri awali ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu. Hata hivyo uchaguzi huo umeakhirishwa hadi wakati mwingine baada ya Mahakama Kuu ya nchi hiyo kupinga wakati huo uliokuwa umeainishwa. Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa uchaguzi wa bunge huwenda ukafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Duru nyingi za kisiasa zimesema kuwa zinataraji uchaguzi huo utafanyika kabla ya kumalizika mwaka huu wa 2013 kwa baada ya kuidhinishwa sheria ya uchaguzi na bunge la Misri. Pamoja na hayo yote Abdulghaffar Shukr mwanachama wa Muungano wa Waliberali wa mrengo wa kushoto wa Misri ametangaza kuwa muungano wao unapinga sheria hiyo na kwamba ni jambo lililo mbali kwamba Mahakama Kuu ya Misri itapasisha sheria hiyo. Harakati ya Ukombozi wa Kitaifa pia imeitaja sheria hiyo mpya ya uchaguzi kuwa ni dhidi ya matakwa ya wananchi wa Misri.
Wakati huo huo baadhi ya habari zinasema kuwa Rais Muhammad Mursi ameanza kufanya mashauriano na wapinzani ili kuifanyia mabadiliko serikali ya Cairo.
Gazeti la al Masriyun vile vile limetangaza habari ya kufanyika mazungumzo kati ya ofisi ya Rais wa Misri na vyama viwili vya Congres na al Wafd kuhusu uwezekano wa kuvunjwa serikali ya Hisham Qandil na kuundwa serikali nyingine itakayoongozwa na shakhsia wa kitaifa. Kuvunjwa serikali ya Waziri Mkuu Hisham Qandil, kufutwa kazi Mwendesha Mashtaka mpya na kufanyiwa marekebisho baadhi ya vipengee vya Katiba ni kati ya matakwa ya Harakati ya Ukombozi wa Kitaifa ya Misri inayoundwa na vyama kadhaa na makundi ya kisiasa ya kiliberali, mrengo wa kushoto na ya kisekulari.
Baadhi ya duru za karibu na Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri zimefichua kwamba, Waziri wa Huduma za Chakula Basim Auda na Usama Yasin ni miongoni mwa shakhsia ambao wanatajwa kuwa huenda wakachukua nafasi ya Waziri Mkuu wa sasa iwapo serikali ya Hisham Qandil itabadishwa. Imeelezwa pia kuwa Ikhwanul Muslimin imekitaka chama cha al Wafd kuarifisha majina ya watu watatu watakaogombea nafasi ya Waziri Mkuu. Mabadiliko hayo ni katika juhudi za serikali ya Cairo za kuyashawishi makundi mbalimbali ya kisiasa ili yashirikiane na serikali ya sasa ya Rais Mursi. Katika siku za hivi karibuni Misri imekuwa ikikabiliwa na mivutano mingi huku maandamano na mapigano yakiendelea katika baadhi ya miji ya nchi hiyo ikiwemo Cairo. Duru za habari za kieneo zimeripoti kuwa wapinzani wa Rais Muhammad Mursi jana aliishambulia Ikulu ya Rais katika mji wa Cairo ambapo watu watano waliokuwa wakiandamana walirusha mabaruti ndani ya uwanja wa ikulu ya al Ittihadiyah. Shambulio hilo lilitokea huku baadhi ya makundi ya kisiasa yakilielekezea kidole cha tuhuma jeshi la Misri.
Hata hivyo Rais Muhammad Mursi amepinga tuhuma hizo na kusema kuwa jeshi la Misri siku zote liko pamoja na wananchi. Jenerali Abdulfatah al Sisi pia amesema kuwa jeshi la nchi hiyo ni aminifu na kwamba halijachukua hatua yoyote dhidi ya wananchi tangu kuanza mapambano ya kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Hosni Mubarak.

No comments:
Post a Comment