Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 29, 2012

Watu 3000 wauawa na ndege za Marekani ndani ya miaka 7 nchini Pakistan

Wakili mmoja wa kutetea haki za binadamu nchini Pakistan amesema kuwa, kwa akali watu wapatao 3000 wameuawa nchini humo katika kipindi cha miaka saba iliyopita, kutokana na mashambulizi yanayofanywa na ndege zisizo na rubani za Marekani katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.
Shahzad Akbar mkuu wa taasisi inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu ameiambia televisheni ya Press TV kuwa, watu 170 kati ya 3000 waliouawa na mashambulizi hayo walikuwa ni wanamgambo wa makundi ya kigaidi huku idadi iliyosalia wakiwa ni raia wasio na hatia.
Rais wa Marekani Barack Obama kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana alikiri wazi wazi kuwepo mashambulizi yanayofanywa na ndege zisizo na rubani za Marekani nchini Pakistan. Obama aidha alikiri kuwa, baadhi ya mashambulizo hayo yalifanywa katika maeneo ya raia.

No comments: