Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 29, 2012

Polisi 10 wauawa kwa mlipuko nchini Afghanistan

Habari zinasema kuwa, mlipuko wa bomu la kutegwa uliotokea kando na bara bara umepelekea kuuawa polisi kumi nchini Afghanistan.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Afghanistan Abdul Qayyum Boq Uwi ameiambia Press TV, kuwa, mlipuko ulitokea eneo lililo umbali wa kilometa 80 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Kabul eneo hilo.
Mlipuko huo umetokea huku magari yakipita katika eneo hilo kutokea eneo kulikokuwa na sherehe za ufunguzi wa mradi wa maendeleo.
Wanamgambo wa kundi la Taliban tayari wametangaza kuhusika na mlipuko huo.
Mabomu ya kutengwa kando ya barabara ni moja ya mbinu zinazotumiwa na wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan.

No comments: