![]() |
| Raila Odinga - Waziri Mkuu wa Kenya |
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amesema kuwa nchi yake inafanya juhudi
za kuepusha vita vipya kati ya Sudan na Sudan Kusini. Kiongozi huyo
amesema kuwa iwapo vita kati ya nchi hizo mbili vitazuka upya, basi eneo
zima la Mashariki mwa Afrika litatikiswa kiusalama.
Odinga amekumbusha kwamba nchi za eneo hilo kwa sasa zinakabiliwa na changamoto nyingi yakiwemo masuala ya wakimbizi na ugaidi na kwamba vita kati ya Sudan na Sudan Kusini vitakuwa sawa na kuweka msumari wa moto kwenye kidonda.
Waziri Mkuu wa Kenya amesema hayo alipokutana na ujumbe wa Sudan Kusini mjini Nairobi. Ujumbe huo umewajumuisha mawaziri na maafisa wengine wa ngazi za juu wa serikali ya Juba.
Sudan na Sudan Kusini zimekuwa zikinyoosheana kidole cha lawama katika siku za hivi karibuni kuhusiana na mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo la mpaka wa pande mbili hizo.

No comments:
Post a Comment