Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, February 19, 2012

Makundi yenye misimamo mikali Ufaransa yabomoa makaburi Waislamu

Chuki dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa zinazidi kuongezeka baada ya makaburi ya Waislamu kushambuliwa na makundi yenye misimimamo ya kupindukia mpaka. Taarifa zinasema kwamba, watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa fikra za kufurutu ada na ambao wana chuki na Uislamu wameyashambulia makaburi ya Waislamu katika eneo la Aisne nchini humo. Makaburi yapatayo 70 hadi 100 yameharibiwa katika shambulio hilo la chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Ufaransa.
Uchunguzi kuhusiana na tukio hilo umeanza kufanywa na polisi ya nchi hiyo. Wafuasi wa makundi na vyama vya kufurutu ada nchini Ufaransa ni miongoni mwa wafuasi wa mrengo wenye misimamo ya utaifa ambao kikawaida ndio ambao huhusika na vitendo kama hivi. Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waisalamu nchini Ufaransa vimeongezeka mno katika siku za karibuni.

No comments: