Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, February 19, 2012

Jeshi la Libya kutumwa kusini mwa nchi ili kuhitimisha mapigano ya kikabila

Jeshi la Libya lina mpango wa kutuma wanajeshi kusini mwa nchi hiyo kwa shabaha ya kuhitimisha mapigano ya kikabila katika maeneo hayo. Yusuf al-Manqoush Kamanda Mkuu wa Majeshi ya Libya ametangaza kwamba, wanajeshi wa nchi hiyo watatumwa kusini mashariki mwa Libya ili kuhitimisha mapigano ya kikabiliana ya kugombea ardhi. Jenerali Manqoush amesema, kuna taarifa kwamba, idadi ya watu wanaouawa katika mapigano hayo inaongezeka siku baada ya siku na kwamba, uamuzi wa kutuma wanajeshi katika eneo hilo unatokana na sababu hiyo. Makabila ya maeneo ya kusini mashariki mwa Libya yametangaza kwamba, makumi ya watu wameuawa hadi sasa kufuatia mapigano hayo. Hadi sasa Baraza Kitaifa la Mpito la Libya NTC limeshindwa kudhibiti hali ya mambo nchini humo na hali hiyo imepelekea Libya iendelee kushuhudia machafuko katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

No comments: