Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetoa kibali cha kufanyika
uchunguzi kuhusu mapigano ya umwagaji damu yaliyotokea miaka kadhaa
iliyopita nchini Ivory Coast.
Mahakama ya ICC imetangaza kuwa majaji
wa mahakama hiyo wametoa kibali kipya cha kufanyika uchunguzi kuhusu
mauaji ya Ivory Coast. Kibali hicho kinampa Mwendesha Mashtaka wa ICC
haki ya kufanya uchunguzi nchini Ivory Coast kuhusu jinai dhidi ya
binadamu na jinai za kivita zilizofanyika nchini humo baada ya mwaka
2002.
Kutolewa kibali hicho huenda kukapelekea kutiwa mbaroni
watuhumiwa wengine wa mauaji na machafuko ya Ivory Coast hususan wafuasi
wa Rais wa sasa wa nchi hiyo Alassane Ouattara.
Awali Mahakama ya
Kimataifa ya Jinai ilikuwa imetoa kibali cha kufanyika uchunguzi kuhusu
jinai ziliofanyika baada ya tarehe 28 Novemba mwaka 2010 na matukio
yaliyofuatia uamuzi wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo wa
kukataa kukabidhi madaraka ya nchi kwa rais mpya wa nchi hiyo. Zaidi ya
watu elfu tatu waliuawa na malaki ya wengine kukimbia makazi yao katika
machafuko hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment