Shambulio la watu wenye silaha katika jela moja huko kusini mwa Nigeria,
limesababisha makumi ya wafungwa kutoweka. Maafisa wa Nigeria
wametangaza kuwa, tukio hilo lilitokea jana katika jela moja ya mji wa
Akure, kusini mwa nchi hiyo na kuwatorosha wafungwa wapatao 175. Aidha
kwa mujibu wa ripoti hiyo, watu 2 waliuawa na wengine kujerihiwa. Habari
zaidi zinasema kuwa, kulitumika mabomu na silaha nzito katika shambulio
hilo. Hii ni katika hali ambayo katika miezi ya hivi karibuni,
wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamekuwa wakitekeleza mashambulizi
katika jela kadhaa katika miji mbalimbali ya Nigeria.
Kabla ya hapo pia
maafisa wa jeshi la nchi hiyo, walitangaza kuawa watu 22 wakiwemo polisi
wawili na wapiganaji wa Boko Haram wapatao 20 huko mjini Maiduguri
katika mkoa wa Borno nchini humo. Terehe 14 Mei mwaka huu, Rais Goodluck
Jonathan wa Nigeria alitangaza hali ya hatari katika majimbo ya Borno,
Yobe na Adamawa, baada ya wapiganaji wa Boko Haram kutangaza vita dhidi
ya serikali yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment