Rais Barack Obama wa Marekani, anatarajia kuwasili saa nane mchana
nchini Tanzani kwa ziara rasmi ya siku mbili. Tanzania ni miongoni mwa
nchi za Afrika zilizotembelewa tayari na Rais Obama. Hata hivyo wananchi
wengi wa Tanzania wamelalamikia safari hiyo, kutokana na kuzorota
shughuli zao za kijamii kwa muda wa wiki moja sasa.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Obama anayeongozana na familia yake anatarajiwa kupokelewa
jijini Dar es Salaam na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete na baadaye
kwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi. Hapo juzi polisi nchini Afrika Kusini
walipambana na waandamanaji waliokuwa na hasira ambao waliteketeza moto
picha za rais huyo wa Marekani alipokuwa safarini nchini humo.
Waandamanaji hao pia waliteketeza moto bendera za Marekani katika
maandamano hayo yaliyofanyika nje ya Chuo Kikuu cha Johannesburg, tawi
la Soweto, sehemu ambayo Obama aliwahutubia wanafunzi. Akiwa nchini
Senegal Rais Macky Sall wa nchi hiyo alimwambia kinagaubaga Obama kuwa,
nchi yake haiko tayari kuruhusu ushoga na maingiliano ya ngono kati ya
watu wa jinsia moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment