Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia ametaka yafanyike mazungumzo kati ya
nchi yake na Misri juu ya tofauti za ujenzi wa bwawa la Renaissance.
Tedros Adhanom Ghebreyesus ameyasema hayo katika kikao cha pamoja na
waandishi wa habari kati yake na Murad Mudallis waziri mwenzake wa Mambo
ya Nje wa Algeria na kuongeza kuwa, nchi yake inataka kumaliza baadhi
ya tofauti zilizosalia kuhusiana na kadhia hiyo. Aidha Ghebreyesus
ameongeza kuwa, hivi karibuni atafanya safari nchini Misri kuitikia wito
wa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo Mohamed Kamel Amr
kuhusiana na kadhia hiyo.
Hatua ya Ethiopia ya kutaka kujenga bwawa la
Renaissance katika mto Nile, ilikabiliwa na radiamali kali ya srikali ya
Cairo na kuibua suutafahumu kati ya nchi mbili hizo. Misri inaitaka
serikali ya Addis Ababa kufungamana na mkataba wa zamani kuhusiana na
utumiaji wa maji ya mto huo, mkataba ambao unaipa zaidi Misri na Sudan
haki ya kustafidi na maji ya mto huo, suala linalopingwa na Ethiopia
inayosisitiza juu ya mkataba wa Entebbe, Uganda unaozipa haki sawa nchi
zote zinazochangia maji ya mto huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment