Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, July 1, 2013

Nane wajeruhiwa kwa risasi Brooklyn Marekani

Watu wasiopungua wanane wamejeruhiwa baada mwanaume mmoja kufaytua risasi katika eneo la makazi ya raia huko Brooklyn mjini New York, Marekani. Ufyatuaji risasi huo umetokea leo asubuhi huko East Flatbush. Wanaume wanne na wanawake wanne ni miongoni mwa majeruhi ambao walikimbizwa katika hospitali za karibu baada ya tukio hilo. Mtu mmoja kati ya hao amejeruhiwa vibaya sana na hali yake imeripotiwa kuwa mbaya. Hadi sasa hakuna mtu yoyote aliyetiwa nguvuni kuhusiana na ufyatuaji risasi huo uliofanywa mapema leo asubuhi.
Ufyatuaji risasi ulitokea leo huko Brooklyn umejiri ikiwa zimepita siku chache tu baada ya watu wengine saba kuuawa na wengine 29 kujeruhiwa katika tukio kama hilo huko Chicago. Takwimu za FBI zinaonyesha kuwa watu 8583 waliuliwa kwa risasi nchini Marekani mwaka juzi, kiwango ambacho ni sawa na kuuawa watu 24 kwa siku.

No comments: