Msemaji wa Rais Muhammad Mursi wa Misri amesema kuwa, mazungumzo ndiyo
njia pekee ya kuiepusha nchi hiyo na mgogoro wa kisiasa. Ehab Fahmy
amefafanua kuwa, ikulu ya rais imejiandaa kufanya mazungumzo ya kitaifa
na ya kweli. Aidha Ehab amewataka wapinzani kufanya maandamano ya amani.
Kwa upande mwingine msemaji huyo wa rais ametangaza kuwa, Rais Muhammad
Mursi amekiri kufanya baadhi ya makosa na kuahidi kuyarekebisha.
Rais
Mursi amenukuliwa akisema kuwa, Misri haitoshuhudia mapinduzi mengine
wala uchaguzi wa mapema. Mursi ameyasema hayo, alipokuwa akiongea na
mwandishi wa habari wa gazeti la The Guardian na kuwataka wapinzani
wake, kuacha maandamano. Hii ni katika hali ambayo mamilioni ya Wamisri
wenye hasira wanaendelea kufanya maandamano makubwa katika maeneo
mbalimbali ya nchi hiyo wakimtaka Rais Muhammad Morsi ajiuzulu na
kuitisha uchaguzi wa kabla ya wakati. Katika upande mwingine, maelfu ya
wafuasi wa Morsi nao wameandamana wakimtaka rais huyo aendelee kusalia
madarakani kwa hoja kuwa amechaguliwa kihalali na wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment