Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wa Yemen amemtaka rais aliyeenguliwa
madarakani Ali Abdullah Saleh, kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi
hiyo. Rais Abd Rabbuh Mansur amekosoa vikali matamshi ya Saleh dikteta
wa zamani wa Yemen aliyesema kuwa, hivi sasa nchi hiyo haina amani na
utulivu na kuongeza kuwa, ikiwa dikteta huyo hatoacha mwenendo wake huo,
basi atafichua faili la ufisadi mkubwa wa viongozi wa utawala wake
uliopita.
Aidha Saleh sambamba na kukosoa serikali ya sasa ya Abd Rabbuh
Mansur Hadi kuwa haina uwezo wa kuongoza, ameituhumu pia kwa kushindwa
kurejesha amani na utulivu nchini. Rais Abd Rabbuh Mansur alishika
hatamu za uongozi wa Yemen kutoka kwa Ali Abdullah Saleh mnamo tarehe 21
Februari mwaka 2012 kwa mujibu wa makubaliano ya kukabidhi madaraka,
yaliyofanyika kwa mpango wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi.
Hivi sasa rais huyo anakabiliwa na changamoto nyingi hususan madai ya
kujitenga kusini mwa nchi hiyo, kuendelea kupenyeza serikalini wafuasi
wa Saleh na kukosekana usalama kunakosababishwa na kuwepo wanamgambo wa
Al-Qaida nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment