Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail
Showing posts with label Mawakili wa Takukuru watinga Kortini nusu uchi. Show all posts
Showing posts with label Mawakili wa Takukuru watinga Kortini nusu uchi. Show all posts

Friday, January 25, 2013

Mawakili wa Takukuru watinga Kortini nusu uchi

WAKILI wa Kujitegemea Ademba Gomba aliwaumbua waendesha mashtaka wawili wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kuiomba Mahakama isiwatambue uwakilishi wao, hadi wakavae vizuri.
Omary The Great ilishuhudia mawakili hao wa kike, Hellen Osujaki  na Faraja Sambala wakitinga Mahakamani wakiwa wamevaa nusu uchi hususan sehemu za vifuani zikionekana hata jinsi cheni zao zilivyokuwa zimekaa ilikuwa ni aibu tumu.
Kabla ya kesi kuanza watu waliokuwa katika Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiwemo washtakiwa walishindwa kuvumilia  aibu hiyo kiasi cha kuguna na kusema "Duh aibu gani hii".
Kitendo hicho kilimfanya Wakili  Ademba aiombe  Mahakama isitambue uwepo wa uwakilishi wa mawakili hao wa Takukuru Mahakamani hadi hapo watakaporekebisha mavazi yao kwa kuvihifadhi vifua vyao.