Kamati ya kuutafuta mwezi mwandamo katika Ofisi ya Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa, Siku kuu ya Idul Fitr
itaadhimishwa kesho nchini Iran na kwa msingi huo Ijumaa ya leo ni siku
ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini.
Ofisi hiyo imetoa taarifa na kusema kuwa, Alhamisi jioni mwezi
mwandamo haukuonekana na kwa msingi huo Ijumaa hii ni siku ya mwisho ya
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kesho, ni Idul Fitr, Inshaallah.
Serikali ya Oman pia imetangaza kuwa mwezi haukuandama jana Alkhamisi
na kwa hivyo Idul Fitr itaadhimishwa kesho nchini humo. Afghanistan na
Morocco pia ni kati ya nchi ambazo Idul Fitr itaadhimishwa kesho. Pamoja
na hayo baadhi ya nchi kama vile Syria, Saudi Arabia, Misri, Qatar na
Indonesia zimetangaza Ijumaa ya leo kuwa ni Idul Fitr.
Nchini Kenya Kadhi Mkuu Sheikh Ahmed Muhdhar jana Alkhamisi pia
alitangaza kuwa Waislamu nchini wataadhimisha Idul Fitr Siku ya
Jumamosi. Akizungumza mjini Mombasa, amesema mwezi haukuandama eneo la
pwani kama ambavyo pia haujaandama maeneo mengine ya Afrika Mashariki
hasa Tanzania na Zanzibar.







No comments:
Post a Comment