Vyama vya upinzani vya Bahrain vimesema kuwa vitasusia uchaguzi
wa bunge na mabaraza ya miji, uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba. Taarifa
iliyotolewa na vyama hivyo imesema kuwa, havitoshiriki katika uchaguzi
huo bila ya kufikiwa makubaliano ya wazi ya kisiasa yanayoakisi matakwa
ya wananchi.
Tarifa hiyo iliyotolewa baada ya kufanyika mkutano katika
makao makuu ya mrengo wa upinzani wa al Wefaq imeeleza kwamba, uchaguzi
huo unapasa kuchagua serikali iliyoteuliwa kwa mujibu wa matakwa ya
wananchi na kwamba upinzani utaendelea na harakati za amani za kupigania
demokrasia.
Tangu mwaka 2011 maelfu ya wananchi wanaotaka demokrasia na mageuzi
nchini Bahrain wamekuwa wakiandamana nchini humo, wakitaka utawala wa
kifalme wa Aal Khalifa uondoke madarakani. Waandamanaji hao wamekuwa
wakikandamizwa na vikosi vya usalama na kutiwa mbaroni.







No comments:
Post a Comment