Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Sunday, April 14, 2013

Russia kupinga azimio dhidi ya Syria UN

Sergei Lavrog - Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema Moscow itapinga azimio linalotarajiwa kuwasilishwa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa dhidi ya Syria. Taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa, rasimu ya azimio hilo inaonyesha mambo mengi ya uongo kuhusu kadhia ya Syria. Taarifa hiyo imefafanua kwamba azimio hilo linaituhumu serikali ya Rais Bashar Asad kuwa ndiyo yenye kusababisha mauaji na ghasia bila ya kutaja nafasi ya makundi ya kigaidi katika mgogoro huo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imehoji ni kwa nini azimio hilo halizungumzii jinsi magaidi wa Syria wanavyowaua raia wa kawaida kila siku.
Russia pia imesema azimio hilo linalenga kupindua serikali halali ya Syria iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia. Tayari Russia imepinga maazimio mawili dhidi ya Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika siku za huko nyuma.

No comments: