Muhammed Malik, ambaye pia ni mwanaharakati wa haki za binaadamu wa mjini California, Marekani, ameiambia televisheni ya Press TV kwamba, viongozi wa nchi hiyo wanashughulishwa zaidi na masuala ya vita na hivyo kutolitilia maanani inavyotakiwa suala la uchumi wa nchi yao na ndio maana uchumi wa Marekani unazidi kuporomoka siku baada ya siku.
Mwanaharakati huyo wa haki za binaadamu wa Marekani ameongeza kuwa, badala ya viongozi wa Marekani kuingilia masuala ya mataifa mengine, wanapaswa kufikiria kwanza matatizo ya watu wao.
Amesema, siasa za Marekani za kutenga fedha nyingi kupindukia za kuusaidia utawala wa Kizayuni na kuiongoza kiukandamizaji na kipolisi jamii ya Marekani, haziwezi kutibu ugonjwa wa uchumi unaochechemea wa nchi hiyo.






No comments:
Post a Comment