Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran amesema Tehran na Ankara zinapaswa kufanya jitihada za pamoja ili kuzuia uhusiano wa pande mbili usiharibike kutokana na matamshi yanayotolewa na maaafisa wa pande mbili.
Ramin Mehmanparast ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki ni nchi mbili zenye nguvu na taathira kubwa katika eneo, zina historia, utamaduni na itikadi zinazofanana, na vile vile masuala mengi yanayosaidia kuimarisha uhusiano na kukurubisha misimamo ya kisiasa na kimataifa ya nchi mbili hizi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran aidha amesema Tehran siku zote imekuwa ikiweka wazi mitazamo yake na kufanya jitihada za kuimarisha amani na usalama katika eneo hili.
Aidha Mehmanparast amesema, Iran inasisitizia kuimarishwa ushirikiano wa nchi za eneo hili na kupinga uingiliaji wowote wa kigeni katika masuala ya ndani ya nchi nyininginezo suala ambalo ndio msingi wa siasa zake za nje.

No comments:
Post a Comment