Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wametaka kukomeshwa mapigano kati ya nchi za Sudan na Sudan Kusini na kutoa wito kwa nchi hizo kutatua hitilafu zao katika meza ya mazungumzo.
Katika mkutano wao mjini Arusha Tanzania, Marais hao wameeleza kusikitishwa kwao na mgogoro wa Sudan na Sudan Kusini. Taarifa iliyotolewa baada ya kikao chao cha siku ya Jumamosi, imesema viongozi hao wataendelea kutafuta amani katika nchi hizo mbili.
Kikao hicho cha Arusha kimehudhuriwa na marais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano, Mwai Kibaki wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda na Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi, Therence Sinunguruza.
Mgogoro wa sasa wa Khartoum na Juba ulianza Aprili 10 pale wanajeshi wa Sudan Kusini walipovamia na kukalia kwa mabavu mji wa Heglig wa Sudan. Mji huo wenye utajiri wa mafuta ulikombolewa na jeshi la Sudan baada ya siku 10. Wakati huo huo Sudan imesema imewatia mbaroni raia wanne wa kigeni waliokuwa wakifanya ujasusi huko Heglig. Waliokamatwa ni raia wa Norway, Uingereza, Afrika Kusini na Sudan Kusini.

No comments:
Post a Comment