Mazungumzo ya faragha ya mapatano ya kitaifa kati ya wawakilishi wa serikali na vyama vya upinzani vya Ivory Coast yameanza tangu jana na kuendelea hadi leo Jumamosi huko katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Grand Bassam. Waziri Mkuu wa Ivory Coast Jeannot Ahoussou-Kouadio amesema kuwa serikali imevialika vyama na makundi yote ya kisiasa ya nchi hiyo kushiriki kwenye mazungumzo hayo. Ahoussou-Kouadio amesema amefurahishwa na hatua ya vyama na mirengo ya kisiasa inayoipinga serikali ya kukubali mwaliko wa kushiriki katika mauzungumzo hayo bila ya masharti wala kufanyika mapatano ya kisiasa.
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa, kufanyika mazungumzo ya mapatano ya kitaifa kati ya serikali na vyama vya upinzani mwaka mmoja baada ya kumalizika mgogoro wa uchaguzi huko Kodivaa, ni sawa na kuanza awamu mpya nchiniu humo. Mgogoro wa Ivory Coast ulianza Novemba mwaka 2010 baada ya kutangazwa matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais na kuendelea hadi tarehe 11 Aprili mwaka jana wakati wa kutiwa mbaroni Gbagbo. Oparesheni ya kijeshi ya pamoja ya vikosi vitiifu kwa Alassane Ouattara, mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Kodivaa wa mwaka 2010 na wanajeshi wa Ufaransa ilipelekea kutiwa nguvuni Laurent Gbagbo. Shakhsia wa kisiasa wa Kodivaa sasa wamefikia natija kwamba wanapaswa kujiepusha na kuzusha migogoro na badala yake washirikiane na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya mustakbali mwema wa nchi yao. Hasa ikitiliwa maanani kuwa vyama vyote vya Ivory Coast kikiwemo chama cha Harakati ya Taifa kwa Ajili ya Ukombozi kinachoongozwa na Rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, pia vinashiriki kwenye mazungumzo hayo.
Rais Alassane Ouattara mwaka jana alionyesha nia njema ya kutaka kufanya mazungumzo na vyama vinavyoipinga serikali na tarehe 29 mwezi Septemba alikutana na kufanya mazungumzo na wafuasi wa Laurent Gbagbo. Wafuasi wa zamani wa Gbagbo katika vyama vya Harakati ya Taifa kwa Ajili ya Ukombozi na Congress ya Taifa kwa Ajili ya Mapambano na Demokrasia, walishiriki pia katika mazungumzo hayo.
Laurent Gbagbo anakabiliwa na tuhuma za kufanya jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu wakati wapinzani wake walipokuwa wakikandamizwa nchini humo, na sasa anasubiri kusikilizwa kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya mjini Hague, Uholanzi. Hatua ya Gbagbo ya kupinga ushindi wa mpinzani wake Alassane Ouattara katika uchaguzi wa Rais ilichochea mchafuko huko Ivory Coast na nchi hiyo ikakaribia kutumbukia tena vita vya wenyewe kwa wenyewe. Machafuko hayo yalisababisha vifo vya karibu watu elfu tatu.
Kuanza kwa mazungumzo kati ya serikali na vyama vya upinzani huko Ivory Coast kikiwepo pia chama cha Laurent Gbagbo, ni ishara ya kujitokeza mazingira mapya nchini humo yenye lengo la kujenga na kuimarisha demokrasia.
Kuanza kwa mazungumzo kati ya serikali na vyama vya upinzani huko Ivory Coast kikiwepo pia chama cha Laurent Gbagbo, ni ishara ya kujitokeza mazingira mapya nchini humo yenye lengo la kujenga na kuimarisha demokrasia.






No comments:
Post a Comment