Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Tuesday, April 3, 2012

Ajali ya ndege Siberia yaua zaidi ya watu 30

Ndege yaanguka Seberia
Habari kutoka Siberia zinasema kuwa watu 32 wamefariki dunia kufuatia kuanguka kwa ndege waliyokuwa wakisafiria. Watu wengine 14 wamenusurika wakiwa na majeraha.
Habari zaidi zinasema ndege hiyo ya abiria ya shirika la ndege la UT ilianguka muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Roschino. Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana ingawa uchunguzi unaendelea. Wizara ya uchukuzi ya Russia imesema ajali hiyo huenda imesabashwa na hali mbaya ya hewa.
Russia ina historia chungu ya mikasa ya ajali ya ndege na ajali mbaya ya hivi karibuni ni ile ya mwaka 2010 iliyopelekea kufariki dunia Rais wa Poland Lech Kaczynski pamoja na maafisa kadhaa wa serikali yake wakiwemo mawaziri. 

No comments: