Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Monday, February 13, 2012

Rasimu ya hukumu ya kifo dhidi ya mashoga yapelekwa tena bungeni Uganda

Rasimu ya sheria ya hukumu ya kifo dhidi ya wahalifu wa vitendo vya kujamiiana watu wa jinsia moja imewasilishwa tena katika Bunge la Uganda. Msemaji wa Bunge la Uganda Helen Kawesa amesema muswada huo wa ushoga uliwasilishwa jana katika ofisi za Bunge na kupelekwa kwenye kamati inayoshughulikia masuala ya sheria kwa ajili ya uchunguzi. Kamati hiyo itachunguza rasimu hiyo na kuirejesha bungeni kwa ajili ya mjadala rasmi. Kundi moja linalopinga ubaradhuli linaloongozwa na wabunge na viongozi wa kidini limetangaza kuwa limeamua kurejesha tena muswada huo bungeni baada ya kufikishwa kwa mara ya kwanza bungeni hapo mwaka 2009 na mbunge David Bahati wa chama tawala cha NRM. Muswada huo unapendekeza hukumu ya kifo dhidi ya mtu atakayefanya ngono na mtu wa jinsia kama yake kwa mara ya pili au kufanya tendo hilo chafu na watoto au akiwa muathirika wa virusi vya HIV. Rais Barack Obama wa Marekani amepinga rasimu hiyo inayopiga vita uhabithi na vitendo vya kijamiiana watu wa jinsia moja akiitaja kuwa ni yenye kuchukiza!

No comments: