Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, February 11, 2012

Al Shabaab yasema imehusika la mlipuko wa bomu Mugadishu

Kundi la waasi wa al Shabaab limetangaza kwamba ndilo lililotekeleza mlipuko wa bomu uliotokea jana katika Hoteni ya Muna mjini Mogadishu na kuua watu wasiopungua 17. Kundi la al Shabaab limetangaza kuwa shambulio hilo lililenga wabunge kadhaa na makamanda wa jeshi la serikali ya mpito.
Polisi ya Somalia ilitangaza jana kwamba mtu mmoja aliyekuwa na gari lililokuwa limetegwa mabomu alishambulia Hoteli ya Muna inayotumiwa sana na wabunge karibu ya ikulu ya rais na kuua watu kadhaa.
Msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Afrika nchini Somalia amesema gaidi aliyetekeleza shambulio hilo aliwafyatulia risasi watu waliokuwa katika eneo hilo kwanza kabla ya kujilipua kwa bomu.
Shambulizi hilo linatambuliwa kuwa la hivi karibuni kabisa baada ya wapiganaji wa kundi la al Shabaab kuondoka Mogadishu mwaka jana. 

No comments: