Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Wednesday, May 23, 2012

Wamisri wamiminika katika vituo vya kupigia kura kumchagua rais mpya

Vituo vya kupigia kura nchini Misri vimefunguliwa muda mfupi uliopita na habari zinasema tayari maelfu ya watu wamepiga foleni tayari kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wa rais leo Jumatano na kesho Alhamisi.
Uchaguzi huo ambao ni wa kwanza tangu wananchi wampindue Hosni Mubarak mwezi Februari mwaka jana, umewavutia wagombea 13. Hata hivyo ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya Amr Musa ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), Ahmed Shafiq, Waziri Mkuu wa utawala ulioangushwa, Abdul Munim Abul Futuh mgombea binafsi na Mohammad Morsy mgombea wa chama cha Uhuru na Uadilifu ambacho ni tawi la kisiasa la Ikhwanul Muslimin. Uchaguzi huo unatarajiwa kuingia duru ya pili ambayo itafanyika mwezi Juni. 

No comments: