Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, June 14, 2014

Mufti wa wanamgambo wa Daesh auawa nchini Iraq

Idara ya kupambana na ugaidi nchini Iraq imethibitisha kuuawa mufti wa kundi la Dola la Kiislamu la Iraq na Sham kwa kifupi Daesh huko mjini Tikrit nchini humo. Kwa mujibu wa idara hiyo, mufti huyo wa kundi hilo la kigaidi Swaqru an-Naswir, aliuawa katika operesheni ya jeshi la Iraq iliyofanikiwa katika mji huo. Habari zinasema kuwa, operesheni hiyo ilifanyika kwa kutegemea habari za kiintelijensia katika mji huo. Katika operesheni hizo, zaidi ya wanamgambo 150 wa kundi hilo wameuawa na kujeruhiwa mjini hapo.
Jeshi la Iraq kwa kutumia ndege za kivita jana lilililenga mkusanyiko mkubwa wa magaidi hao na kuua wengi kati yao. Aidha jeshi la Iraq hapo jana pia lilifanikiwa kuuangamiza msafara wa magari ya kundi hilo yapatayo 200 uliokuwa ukielekea mji wa Samarra. Hii ni katika hali ambayo, Nour al Maliki Waziri Mkuu wa Iraq amelipa amri jeshi la nchi hiyo kuisafisha miji yote ya Iraq kutokana na uepo wa kundi la Daesh. Kwengineko sheikh mkubwa wa Kisuni amelitaja kundi la Daesh kuwa ni kundi lililopotea na kwamba halina uhusiano wowote na dhehebu la Kisuni. Sheikh Muhammad Amin mmoja wa wajumbe wa Jumuiya ya Maulama wa Iraq ameyasema hayo kupitia kanali ya televisheni ya Sumaria News na kusema kuwa, hii leo Iraq inakabiliwa na hujuma za matakfiri ambao wanatekeleza ajenda za mabwana zao kwa lengo la kuigeuza Iraq kuwa kichaka cha ugaidi.

No comments: