Makamu Mwenyekiti wa chama cha Uhuru na Uadilifu tawi la kisiasa la
Ikhwanul Muslimiin nchini Misri amesema kuwa, suala muhimu hivi sasa ni
kuondolewa utawala mikononi mwa jeshi kurejewshwa serikali ya kisheria
nchini humo. Issam al-Iryan ameweka wazi kuwa, Ikhwanul Muslimiin
haipingi kufanya kazi zake chini ya katiba na kwamba hadi sasa haijawahi
kukiuka sheria yoyote.
Amesema kuwa, hivi sasa juhudi inayofanyika ni
kumrejesha madarakani Muhammad Mursi rais aliyeondolewa madarakani ili
kuweza kurejesha mwenendo wa demokrasia Misri. Aidha akijibu swali
kuhusu safari ya William Joseph Burns Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani mjini Cairo, Misri, al-Iryan amesema kuwa kutokana na hatua ya
jeshi kuvunja bunge, kusimamisha utekelezwaji katiba na kuondolewa
madarakani rais aliyechaguliwa kisheria nchini humo, hawezi kuwa na
imani kwa Rais Barack Obama wa Marekani wala William Burns. Wakati huo
huo, Ahmed El-Muslimani mshauri wa rais wa mpito katika masuala ya
habari nchini Misri, ameyataka makundi yote ya kisiasa kwa ajili ya
maridhiano ya kitaifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment