Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaka Ufaransa isitishe vita inavyoongoza dhidi ya Mali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi
za Kiafrika na Kiarabu Hossein Amir-Abdollahian ametoa wito huo siku ya
Jumatano huku akisisitiza kuwa mipaka na umoja wa Mali unapaswa
kulindwa.
Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inafuatilia kwa karibu
matukio ya Mali na kwamba inasikitika kuona mauaji na kuachwa bila
makao maelfu ya raia wa nchi hiyo. Abdollahian amesema Iran ambayo ni
mwenyekiti wa mzunguko wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za
Upande Wowote NAM iko tayari kurejesha amani na umoja wa mipaka ya Mali.
Januari 11 Ufaransa ilianzisha vita nchini Mali kwa kisingizio cha
kukabiliana na wanamgambo wa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ya
Magharibi mwa Afrika.







No comments:
Post a Comment