Mkutano mkuu wa kila mwaka wa muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini COSATU umeanza leo Jumatatu huku mgomo wa wafanyakazi wa mgodi wa Platinum wa Marikana ukiendelea kulemaza uchumi wa nchi hiyo. Muungano wa COSATU ambao ni muitifaki mkubwa wa chama tawala nchini humo ANC unatarajiwa kuishinikiza serikali kutatua matatizo ya wafanyakazi wa mgodi huyo wa Marikana haraka iwezekanavyo. Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya vyama vya wafanyakazi nchini humo vimejiondoa chini ya mwavuli wa COSATU baada ya kubainika kuwa muungano huo umeshindwa kusimama imara mbele ya serikali ya ANC na kutetea maslahi ya wafanyakazi. Uchaguzi wa ndani wa muungano huo unatarajiwa kufanyika katika siku ya nne ya mkutano huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







No comments:
Post a Comment