| Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva jana Mei 31 katika siku ya kimataifa ya kukabiliana na matumizi ya tumbaku, mkurugenzi wa mradi wa WHO wa kuwa huru na tumbaku Douglas Bettcher amesema WHO inakadiria kwamba ifikapo mwaka 2030 tumbaku itaangamiza maisha ya watu milioni 8 kila mwaka. Ameongeza kuwa vifo vinne kati ya vitano kutokana na uvutaji sigara huripotiwa katika nchi za kipato cha chini na cha wastani. Tumbaku imetajwa kuwa chachu kubwa ya maradhi yasiyo ya kuambukiza kama saratani, magonjwa ya moyo, kisukari na matatizo ya kupumua. WHO imetoa wito kwa serikali duniani kuchukua tahadhari kwani mashirika ya utengenezaji sigara yanajaribu kuzuia kampeni za kuwashawishi watu wasivute sigara. |
Friday, June 1, 2012
WHO yasema tumbaku huua watu milioni 6 kila mwaka
Posted by
AO Secretarial & Technology Supplies
Subscribe to:
Post Comments (Atom)






No comments:
Post a Comment