Uhuru Kenyatta, William Ruto, Francis Muthaura na Joshua Sang wanatuhumiwa kuhusika kwa njia moja au nyingine katika machafuko hayo ya baada ya uchaguzi mkuu wa Rais uliofanyika Disemba mwaka 2007. Kwenye machafuko hayo yaliyoendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2008, takriban watu 1300 waliuawa na mamia ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao na hivyo kulazimika kuwa wakimbizi wa ndani. Kwenye uchaguzi huo, ushindani mkali ulikuwa kati ya Raila Odinga wa chama cha ODM na Rais Mwai Kibaki wa PNU. Machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu huo yalichochewa zaidi na uhasama kati ya wafuasi wa viongozi hao wawili. Baadaye harakati za upatanishi zilizoongozwa na Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa zilizaa matunda ambapo Mwai Kibaki pamoja na Raila Odinga walikubaliana kugawana madaraka na hivyo kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Saturday, May 26, 2012
Kupandishwa kizimbani washukiwa wanne wa machafuko ya kisiasa ya 2007 nchini Kenya katika mahakama ya ICC
Uhuru Kenyatta, William Ruto, Francis Muthaura na Joshua Sang wanatuhumiwa kuhusika kwa njia moja au nyingine katika machafuko hayo ya baada ya uchaguzi mkuu wa Rais uliofanyika Disemba mwaka 2007. Kwenye machafuko hayo yaliyoendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2008, takriban watu 1300 waliuawa na mamia ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao na hivyo kulazimika kuwa wakimbizi wa ndani. Kwenye uchaguzi huo, ushindani mkali ulikuwa kati ya Raila Odinga wa chama cha ODM na Rais Mwai Kibaki wa PNU. Machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu huo yalichochewa zaidi na uhasama kati ya wafuasi wa viongozi hao wawili. Baadaye harakati za upatanishi zilizoongozwa na Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa zilizaa matunda ambapo Mwai Kibaki pamoja na Raila Odinga walikubaliana kugawana madaraka na hivyo kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Posted by
AO Secretarial & Technology Supplies
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment